Majukumu ya Baraza
Majukumu ya Baraza
Baraza la Ushindani ni Taasisi maalum na huru ya rufaa ambayo imekusanya utaalamu wa kiuchumi, biashara na sheria kwenye utekelezaji wa majukumu yake ya msingi ambayo ni kupokea, kusikiliza na kutolea maamuzi kesi/mashauri yote ya rufaa yanayohusu Ushindani wa kibiashara na udhibiti wa Soko kutoka kwenye Tume ya Ushindani (FCC) na Mamlaka za Udhibiti zifuatazo:
- Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (EWURA)
- Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (LATRA);
- Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Anga (TCAA);
- Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA); na
- Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA).
Maamuzi ya Baraza hili ni ya mwisho katika mfumo mzima wa Ushindani na udhibiti wa Soko.