Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara

Mwenyekiti na wajumbe wa Baraza wanapatikanaje?

Mwenyekiti anateuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushauriana na Jaji Mkuu na anapaswa kuwa miongoni mwa Majaji wa Mahakama Kuu. Wajumbe wanateuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka kwenye majina yaliyopendekezwa na Kamati ya Uteuzi.