Habari

Rais Samia ateua Wajumbe 6 Baraza la Ushindani
  • 14 Sep, 2021
Rais Samia ateua Wajumbe 6 Baraza la Ushindani

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewateua wajumbe sita (6) wa Baraza la Ushindani (Fair Competition Tribunal- FCT) kwa mujibu wa kifungu cha 83(2) (b) cha Sheria ya Ushindani (The Fair Competitionn Act).

Wajumbe walioteuliwa ni kama ifuatavyo:

1. Dkt. Onesmo Michael Kyauke kutoka Locus Attoneys;

2. Prof. Honest Prosper Ngowi kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe;

3. Dkt. Hanifa Twaha Masawe kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe;

4. Mhandisi Bonifasi Gissima Nyamo-Hanga kutoka Wakala wa Majengo Tanzania;

5. Dkt. Godwill George Wanga kutoka Baraza la Taifa la Biashara;

6. Dkt. Neema Bhoke Mwita kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino .

Uteuzi wa Wajumbe hao utadumu kwa kipindi cha miaka mitatu (3) kuanzia tarehe 16, Juni, 2021.